Jumatano, Septemba 21

TAHADHARI KWA WENYE MATATIZO YA PUMU(ASTHMA)

Pumu ni miongoni mwa magonjwa sugu ya hewa yanayosumbua  idadi kubwa ya watu Duniani hasahasa watoto.
   Tatizo hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku,

Makala hii fupi inakusudia kutoa Tahadhari ambazo yapasa zichukuliwe kwa mwenye tatizo la pumu.


1.Epuka maeneo  yanayochochea shambulizi la pumu kwako kutokana na maelezo ya DAKTARI.

2.EPUKA VIPODOZI NA MANUKATO YENYE HARUFU KALI ambayo yanachochea pumu kwa upande wako.

3.Kula vyakulavyenye asili ya mboga za Majani kama vile nyanya, matango maharagwe mabichi, bilinganya na vyakula vingine vyenye asili hii.


4.MGONJWA ANAPASWA ATUMIE SAMAKI WABICHI KWA WINGI.


MAAJABU YA MASSAGE KATIKA MAGONJWA HATARISHI

.
Massage(Uchuaji)  ni tiba kongwe na ya uhakika katika kutibu magonjwa mbalimbali,kuanzia ya mwili na hata ya akili.Tiba hii ya massage huleta matokeo chanya pale itakapotolewa na Mtaalamu(Massage Therapist). Magonjwa mbalmbali tangu kale yamekuwa yakitibiwa na bado  hadi leo inaendelea kufanya kazi huku Wataalamu wakifanya tafiti mbalimbali ili kuzidi kuiboresha zaidi. Faida kubwa ya tba hii ni kwamba haina athari mbaya za kikemikali kwani dawa nyingi zinazotumika ni za asili (Organic).Miti mbalimbali hutumika katika kutengeneza mafuta yanayotumika kufanya massage.


Kuna magonjwa hatari ambayo yanaweza kutibika kupitia Massage. Hatari kubwa iliyopo ni kwamba watu wengi (hasa hapa Tanzania) huichukulia Massage kwa Mtazamo hasi na hii huwafanya wakose hata kufahamu kuwa massage ina umuhimu mkubwa katika Maisha yao.

Yafuatayo ni Magonjwa ambayo Massage imeonyesha Msaada Mkubwa katika kufanikisha kuyatibu. Na hii hutokana na Mbinu za kitaalamu zinazozifanywa  na watoaji wa huduma hii. Massage imeonyesha Msaada mkubwa katika kufanikisha kutibu Magonjwa yafuatayo.


1.MAGONJWA YA AKILI

Massage imeonyesha msaada mkubwa sana katika kutibu Magonjwa ya Akili.  Massage huamsha seli za ubongo na kuzifanya ziweze kufanya kazi katika hali iliyo nzuri. Hii ni kwa sababu magonjwa mengi ya akili tatizo huwa ni katika seli za ubongo ambazo hushindwa kupokea taarifa vilivyo kutoka katika Milango ya fahamu.

2.MAGONJWA YA KANSA

Kansa husababishwa na seli zisizo za kawaida katika mwili. Seli hizi zikiendelea kuwepo huziambukiza seli nyingine na hivyo kuongeza madhara zaidi. Suluhisho pekee ni kuziondoa seli hizo, Kwa sasa kuna Teknolojia ya kuziua Seli hizo zisizo za kawaida ili zisilete madhara zaidi. Massage ni njia bora kabisa ya kuharakisha kuziteketeza seli hizo. Hivyo kwa watu wenye Matatizo hayo ni vema wapate huduma ya massage itawasaidia.


3.MAGONJWA YA VIUNGO

Magonjwa mengi ya Viungo vya mwili yanatibika kiurahisi kupitia Massage. Uvimbe, kukaza kwa misuli, kukaza kwa viungo(joints) ni miongoni mwa Magonjwa yanayoweza kutibika kupitia massage.


4.KIHARUSI(STROKE)

Ugonjwa huu hutokea pale ambapo neva zinazosafirisha taarifa mwilini zinapokufa au kusimama kufanya kazi, Hali hii husababisha kukata kabisa kwa Mawasiliano kati ya Milango ya fahamu na Ubongo. Hivyo husababisha Mtu kushindwa kutumia hata viungo vyake kwa kuwa hakuna tena mawasiliano. Watu wengi wanapopata tatizo hili hukata tamaa kabisa na kuona kuwa huo ndio mwisho wa Maisha yao.Ukweli halisi ni kwamba , Massage imeonyesha ufanisi mkubwa katika kuharakisha Uponaji wa Tatizo hili. Kama mgonjwa atawahishwa. Kazi kubwa ya massage katika tatizo hili la kupooza ni kuamsha neva zilizolala ili ziendelee kufanya kazi kama kawaida. 

BEI ZETU NI SAWA NA BURE,
ILI KUPATA HUDUMA HII, FANYA BOOKING KWA KUPIGA SIMU

0715343161
0756343161
0787343161

instagram.com/happinessmassage

Jumatano, Septemba 7

MADHARA YA KUKAA KWA MUDA MREFU.

Habari na karibu mpenzi msomaji wa Happiness Massage Serrvices.
  Kama ilivyo ada ni wajibu wetu kukuelimisha wewe msomaji wetu.
Nianze kwa kutoa shukrani kubwa kwako wewe msomaji wa Blog hii.Tunathamini uwepo wako,Na Tunajitahidi kufany kila njia ili uendelee kupata maarifa mbalimbali.
   Afya ni kitu cha msingi sana katika m,aisha yetu,Hivyo ni lazima tujali Afya zetu ioli kuhakikisha tunaendelea kuwa bora kila siku na hivyo kufurahia Maisha yetu ya kila siku.

Jumanne, Septemba 6

UMUHIMU WA MASSAGE KWA WAZEE



Wazee wakiwa ni watu walio katika hatua ya Mwisho ya Ukuaji Wa Binaadamu huwa wanakutwa na matatizo mbalimbali.Hii inathibitisha kauli isemayo Uzee ni ugonjwa.


Bila kupoteza muda Mpenzi msomaji ningependa kwenda moja kwa moja kueleza Umuhimu wa Massage kwa Wazee kama ifuatavyo.
1.Massage huwapa nguvu wazee na hivyo wanaweza kutembea kirahisi.

2.Massage kwa Wazee huwaondolea hali ya kutetemeka kwa Viungo. Wazee walio wengi wana hali ya kutetemeka kwa viungo kitaalamu inafahamika kama Parkinson's disease. Massage ni tiba bora ya kumaliza tatizo hili.

3.Massage kwa wazee inasaidia kuongeza vilainishi vya viungo.

4.Massage kwa wazee huwasaidia kuondoa kukaza kwa misuli.

Alhamisi, Septemba 1

ITAMBUE THAMANI YA AFYA YAKO


Ni wajibu wetu kukuelimisha juu ya njia bora za kuboresha Afya yako ili iimarike na uweze kuishi kwa furaha, kumbuka afya ni uhai, pasipo afya njema hakuna raha tena ya kuishi. Kila kilichokuwa kwako kizuri na cha kufurahisha kinageuka na kuwa kibaya.

Kwa kulitambua hilo na kuthamini Afya Yako, Happiness Massage tumekusudia Kukusaidia.

Tunatoa huduma bora za Massage zinazolenga kuboresha afya yako na kurejesha Furaha yako ya asili.


 
0756 343 161
0715 343 161

KARIBU SANA HAPPINESS MASSAGE SERVICES.

Jumatatu, Agosti 29

UMUHIMU WA MASSAGE KWA WATOTO



Mtoto ni tunda bora linalotokana na Mti wa Ndoa. WanaNdoa walio wengi Duniani hujikuta katika furaha isiyo na kifani wanapopata Mtoto/Watoto. Wapo wanaosema kuwa Mtoto ni burudisho la Macho ya Wanandoa na hili si Uongo ni kweli kabisa. 

Mtoto  anahitaji apatiwe Huduma nyeti sana ambayo kutokana na huduma hiyo nyeti na muhimu ndiyo itakayomjengea msingi mzuri katika maisha yake yote atakayoishi hapa duniani. Huduma hiyo si nyingine bali ni malezi.  Na si malezi tu bali Ni malezi bora. Malezi yana maana kubwa sana kuanzia Kumpatia mtoto chakula bora, Mavazi, Huduma bora za afya na kuhakikisha kuwa Mtoto anakuwa na furaha, ni miongoni mwa vipengele vya Malezi. 

JE,WAJUA? 
Massage humuongezea Mtoto Furaha na si Hivyo tu, Bali pia Huboresha Afya ya Mtoto. Kama ulikuwa haufahamu basi kuanzia leo fahamu hivyo. Makala hii itajikita zaidi katika Kuzungumzia Umuhimu wa Massage Kwa Mtoto mdogo. Massage ina umuhimu mkubwa katika kuboresha Afya ya Mtoto na Kumuongezea Furaha. 

“Unapomfanyia Mtoto wako Massage,Bila shaka unausisimua Mfumo wa Fahamu”<Maneno haya Yalitamkwa na Dr.Tiffany Field kutoka Taasisi ya Uchunguzi ya Chuo Kikuu cha Miami (Marekani), Katika kitengo cha Shule ya Matibabu. 

Bila kwenda mbali zaidi Massage  humletea mtoto Mambo yafuatayo.

1.Humfanya mtoto apate Usingizi Mzuri. Hii ni kutokana na Masaage hulainisha viungo vyake na kumfanya mtoto awe katika hali nzuri ya kimwili.

2.Inaboresha Afya ya Mtoto. Kama ilivyotanguliwa kuandikwa kwamba Massage kwa mtoto husisimua mfumo wa fahamu. Msisimuko huo wa mfumo wa fahamu husababishwa kuzalishwa kwa Serotonin, ambayo ndiyo huleta furaha.Serotonin ndiyo pia inayosaidia kuongeza raha katika Tendo la Ndoa. Hii husaidia kupunguza mapigo ya moyo kwa mtoto na kumwacha mtoto akiwa na furaha muda wote.


Karibu Happiness Massage Tuboreshe Afya ya mtoto wako na kurejesha furaha yenu.

0715343161

Alhamisi, Agosti 25

JINSI MASSAGE INAVYOTIBU MSONGO WA MAWAZO



Msongo wa mawazo(stress) ni hali inayotokea kwa mtu baada ya kukumbana na tatizo fulani lisilokuwa zuri katika maisha yake. Hali hii humfanya mtu ajisikie mpweke,aliyeuzika na kukosa
furaha kabisa na hata kukosa hamu ya kula.Mara nyingi msongo wa mawazo hutokea kwa Vijana,lakini muda mwingine na kwa wazee pia.Msongo wa mawazo usipopatiwa
Ufumbuzi,hupelekea SIMANZI,ambayo ndiyo hali mbaya zaidi. Watu wengi hupata msongo wa mawazo lakini hawafahamu hali hiyo ndio msongo wa mawazo.Zifuatazo ni Dalili zinazoweza kuashiria msongo wa mawazo. 1.Maumivu ya kichwa 2.Uchovu 3.kukosa hamu ya kula 4.Kujihisi mpweke 5.kushindwa kufanya kazi zako za kawaida.  SABABU ZINAZOPELEKEA MSONGO WA MAWAZO Kuna sababu mbalilmbali zinazopelekea Msongo wa mawazo......
Sababu hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine.Zifuatazo ni sababu zinazopelekea Msongo wa mawazo.
 1.Kufeli Mitiahani Mtu anapopata matokeo mabaya ya mitihani yake kinyume na alivyotarajia anaweza kupata msongo wa mawazo.
 2.Kuondokewa na mzazi/wazazi au mlezi/walezi au mtu wa karibu kama vile mwenza,ndugu, rafiki n.k huweza kumfanya mtu apate msongo wa mawazo.
 3.Usaliti katika Mapenzi Hii ni sababu kubwa kwa vijana inayopelekea msongo wa mawazo.Mtu aliyeasalitiwa huwa katika hali ngumu ya kihisia nahivyo kumfanya apate Msongo wa mawazo.Unapokosekana Ushauri kwa mtu wa namna hii huweza kumfanya achukue maamuzi mazito hata ya kujiua,na hii imeshuhudiwa mara nyingi sana ikitokea.
 4.Matatizo ya kifamilia Panapotokea matatizo ya kifamilia kama vile ugomvi au malumbano na usipofikiwa muafaka huweza kutokea msongo wa mawazo pia. Sababu nyingine zinazopelekea Msongo wa mawazo ni: Mikwaruzano na watu,Hofu ya tukio linalotarajiwa kama vile Mtihani,Kesi Mahakamani n.k. 

ATHARI ZINAZOTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO 
1.KIFO Msongo wa mawazo huweza kupelekea kifo kama mhusika hatochukua hatua za kuiondoa hali hiyo au kama hatopatiwa suluhisho.Mfano mwaka 2013 kuna mwanafunzi aliyejiua kutokana na kupata matokeo asiyoyatarajia katika mtihani wake wa kidato cha nne.Hii bila shaka imetokea na msongo wa mawazo.

2.KUDORORA KWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KIUJUMLA. 
Kutokana na hali aliyokuwa nayo mtu mwenye msongo wa mawazo ni vigumu sana kufanya kazi na hata kama atafanya bado hakutokuwa na ufanisi.Hali hii hupelekea kushuka kwa shughuli za uzalishaji na hivyo huathiri hali ya uchumi.

3.MSONGO WA MAWAZO HUPELEKEA MAJONZI YA MUDA MREFU KWA MUHUSIKA. Kama msongo wa mawazo utaendelea kuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa suluhisho,inaweza kupelekea majonzi ya muda mrefu hali ambayo husababisha afya ya mhusika kuzorota. SULUHISHO LA MSONGO WA MAWAZO. Kabla sijaeleza kuhusu suluhisho la msongo wa mawazo,ningependa ufahamu kwanza.Kuna Njia tofauti zinazotumika kuondoa msongo wa mawazo.Njia hizi hutegmea ukubwa wa msongo wa mawazo. Kwa msongo wa mawazo wa kawida,njia zifuatazo zinaweza kumaliza kabisa tatizo hilo.

1.Massage ni Suluhisho bora kabisa katika  kuondoa Msongo wa mawazo. Kwa nini? Kwa sababu Wataalamu wa Massage(Uchuaji) wana ujuzi wa kutosha wa jinsi ya kushughulika na Mtu Mwenye Msongo wa mawazo kwa njia zote mbili(Kimwili na Kiakili). Na hii ndio tiba bora kwani mtu mwenye Msongo wa mawazo anaathirika kimwili(uchovu/kukosa nguvu) na kiakili.Wataalamu wanaotoa Huduma hizi za Massage(Uchuaji) kama vile Happiness Massage Services wanatumia Maarifa ya Fiziolojia na Saikolojia ili kuleta ufanisi katika tiba hii ya kuondoa Msongo wa Mawazo.Kitu cha kwanza kinachoathirika ni akili na baadae mwili hufuatia. Wataalamu wa Massage Hutumia mbinu muafaka ya kuanza kuondoa tatizo lililopo katika akili(ambalo huwa mawazo, huzuni, kujiisi mpweke, kufikiria mambo mabaya kama vile Kujiua) na baada ya kumweka mtu sawa kiakili Ndipo tiba ya Mwili inafuata.

Njia nyingine za kutatua tatizo hili la msongo wa mawazo n

2.Kutafuta mtu wa kuongea nae badala ya kukaa peke yako.

3.Kufanya mazoezi ya viungo.
Husaidia kuweka akili sawa na hivyo kurudi katika hali ya kawaida.

4.Kula mlo kamili. Mara nyingi mtu mwenye msongo wa mawazo hukosa hamu ya kula, na hali hii ya kukaa bila kula ndio huongeza zaidi tatizo, hivyo inashauriwa kujilazimisha kula. Ikiwa haya yote hayo yamefanyika na hakuna matokeo chanya, Msaada wa kitaalamu unahitajika kwa haraka kabla ya kuleta madhara zaidi.

Jumapili, Agosti 21

HISTORIA YA MASSAGE

HISTORIA YA MASSAGE Historia ya massage(uchuaji) inatokea mbali takribani miaka 5000 iliyopita miaka ambayo massage(uchuaji) ilikuwa ni njia kuu katika matibabu ya magonjwa mbalimbali.Si magonjwa ya viungo tu bali pia hata magonjwa mengine Michoro ya mapangoni inayopatikana sehemu mbalilmbali Duniani ni ishara/dalili tosha inayothibitisha kuwa tiba hii kongwe(ya massage) ilianza miaka

Alhamisi, Agosti 18

HII NDIO DHANA POTOFU KUHUSU MASSAGE

Massage ikiwa kama njia ya kitaalamu ya kuondoa maumivu, uchovu na kutibu magonjwa mbalimbali,lakini bado kuna watu ambao wana mtazamo potofu juu ya massage
Hali hii husababishwa na sababu zifuatazo:
1.Kutokujua maana halisi ya massage  2.Baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa massage ili waweze kuficha MAOVU, (wanayotenda).Watu wa aina hii ndio wanaosababisha massage ionekane kitu kibaya kwa jamii.Na hivyo kuwafanya watu wafikirie kivingine(hasi).

       MASSAGE NI TIBA BORA YA ASILI KATIKA VIUNGO (PHYSIOLOGY)
tiba hii haijaanza mwaka jana au mwaka huu bali ni tiba iliyoanza tangu enzi za kale.

Jumatano, Agosti 17

Ifahamu Deep Tissue Massage.

DEEP TISSUE MASSAGE
Ni massage ya nguvu amabayo wanafanyiwa watu wenye mataizo ya kukaza kwa misuli, hasa wale wanaofanya mazoezi sana.
Massage ya aina hii inalenga  tabaka za chini za ngozi(endodermis na mikano)  ambalo huzunguka misuli,mifupa na viungo.

Sehemu ya juu na chini ya mgongo, na miguu.
UMUHIMU WA DEEP TISSUE MASSAGE.

Fahamu kuhusu kupasuka kwa Nyayo(visigino).sababu na suluhisho.

Kuwa na miguu au visigino vilivyopasuka (gaga au machacha) ni moja ya sababu inayoweza kuonyesha kuwa katika mwili kuna upungufu wa virutubisho kadhaa, vitamini au madini.
Japo wengi wetu tumekuwa na mitazamo kwamba, visigino kupasuka ni ishara ya
mtu kutojali usafi wa miguu yake, ila mpenzi msomaji leo napenda kukushirikisha mambo kadhaa kuhusu mtu kupasuka visigino.
Kwa kawaida, ngozi zetu huwa zina unyevunyevu ambao huiwezesha ngozi ivutike au kutanuka pamoja na kusinyaa bila ya kutokea madhara yoyote kama vile kuchanika. Pamoja na ngozi kugawanyika katika sehemu tatu ( sehemu ya nje

SABABU 10 KWA NINI NI MUHIMU UFANYE MASSAGE

Karibu sana mpenzi msomaji, massage(uchuaji) ni njia iliyo bora katika kutibu magonjwa mbalimbali ya mwili/viungo.Makala hii itakufahamisha umuhimu wa wewe kufanya massage. Watu wengi huchukulia kuwa massage ni maalumu kwa watu fulani tu, kumbe si hivyo.
Zifuatazo ni sababu 10 za msingi ,kwa nini ni muhimu ufanye massage
1.Massage huondoa maumivu ya viungo.
2.Massage  huboresha ujongeaji  wa viungo 

Tiba ya chunusi, Fahamu kwa undani hapa.

  Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wa mataifa yote na wa umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata chunusi. Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana na chunusi.

Massage ya Miguu na Umuhimu wake

Massage ya Miguuni inasaidia kuweka misuli katika hali ya usawa, pia kwa wale waliopooza pia inawasaidia kuhamsha seli(activation of NERVE CELLS) na mishipa ya damu iliokakamaa kwa muda mrefu. Unashauriwa kufanya massage kwa ajili ya afya yako.
Kumbuka kuwa maumivu ya kawaida yakiwa endelevu yanaweza kusababisha matatizo zaidi.
Kwa kuepuka hayo yasitokee. Ni vema ufanye massage mapema.
kwa huduma nzuri za massage na bei nafuu

Jinsi ya Kupunguza uzito kupitia na mafuta mwilini

Single sauna nikifaa kinacho saidia kuondoa sumu mwilini kwa asilimia kubwa kinatoa mafuta(cholesterals) hivyo uta pungua kwa muda mfupi tuu ndani ya siku 7 utaona matokeo makubwa saana haina madhala kwa mtumiaji  itakufanya unywe maji mengi na kupunguza kula vyakula vya mafuta .
Njoo tukuhudumie**
TUNAPATIKANA ILALA,LAMADA HOTEL
Au TUPIGIE
0787 34 31 61
0715 34 31 61
0756 34 31 61
KARIBUNI SANA.

Suluhisho la Maumivu ya Mgongo.

Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo au lumbago ni hali inayotokea mara nyingi kwenye misuli na mifupa ya mgongo. Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao.
Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanaweza kuainishwa kwa urefu kama maumivu makali ya ghafla (yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6),maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inayosababishwa na jeraha au isiyosababishwa na jeraha au maumivu hame .
Katika visa vingi vya maumivu ya mgongo, kisababishi maalum kikuu hakitambuliwi wala kukadiriwa, kwa sababu maumivu huaminika kusababishwa na jeraha kama vile misuli au mkazo wa viungo

Jumanne, Agosti 16

Massage ni nini? Fahamu kuhusu Massage.

Massage(Uchuaji kwa kiswahili) ni usuguaji na ukandaji wa sehemu za mwili(hususani viungo,tishu na misuli) au mwili mzima kwa kutumia mikono kwa lengo la kuondoa uchovu,maumivu au kutibu magonjwa.Massage(Uchuaji) ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kutokana na shughuli endelevu zinazofanywa kila siku na hivyo