Jumanne, Agosti 16

Massage ni nini? Fahamu kuhusu Massage.

Massage(Uchuaji kwa kiswahili) ni usuguaji na ukandaji wa sehemu za mwili(hususani viungo,tishu na misuli) au mwili mzima kwa kutumia mikono kwa lengo la kuondoa uchovu,maumivu au kutibu magonjwa.Massage(Uchuaji) ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kutokana na shughuli endelevu zinazofanywa kila siku na hivyo
kusababisha uchovu,maumivu ya viungo na mwili na hata ugonjwa. Massage inaweza kufanywa na kila mtu(local massage) lakini mra nyingi massage za namna hii haziwi na ufanisi kwa kuwa hazitumii dawa maalumu ya kulainisha viungo/mwili. Fahamu kuwa kufanya massage ni kuuweka mwili wako katika hali nzuri na hivyo kuboresha afya yako.Kukaza k wa misuli kwa muda mrefu kunaweza kusababisha matatizo zaidi.Maumivu ya mgongo yakiwa endelevu pasipo kufanya massage yanaweza kuleta madhara zaidi.
                                                                                                                                                                                                 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni