Sports Massage ni aina ya massage inayolenga kuondoa mikazo ya misuli, maumivu na kuondoa sumu katika misuli ya wanamichezo ili waweze kuongeza ufanisi katika Michezo.
Ili mwanamichezo aweze kuongeza ufanisi ni lazima afanye massage kabla kwa ajili ya muiweka misuli yake imara ili iweze kumudu mikikimikiki ijayo.
Ni muhimu pia baada ya michezo, mwanamichezo afanyiwe massage kwa ajili ya kuipumzisha misuli yake na kuondoa sumu(lactic acid) zilizojikusanya katika seli za misuli.
Muda gani Unashauriwa Kufanya Sports Massage?
Massage kwa mwanamichezo haina muda maalumu, anaweza kufanya massage muda wowote pia ni muhimu zaidi kufanya massage kabla ya mchezo kwa ajili ya kuuweka mwili imara na baada ya massage kwa ajili ya kuipumzisha misuli na kuupumzisha mwili.
Umuhimu wa Massage kwa Wanamichezo
1. Huondoa maumivu katika misuli: Massage inaondoa maumivu yaliyopo katika misuli baada ya mazoezi au mchezo.
2. Huimarisha misuli na kuiweka tayari kwa ajili ya mchezo: Massage husaidia kuondoa ukakamavu wa misuli na kuifanya iwe laini na yenye ufanisi, hivyo humpa nguvu mchezaji ya kukabiliana na mchezo au mazoezi.
3. Huongoza ufanisi wa Mchezaji Uwanjani. Massage kabla ya mchezo humpa nguvu mchezaji, kumuongezea molari na kumuondolea msongo wa mawazo, hivyo mchezaji huwa huru na anategemewa zaidi kuonyesha ufanisi mkubwa kuliko yule asiyefanya massage
4. Huzuia hatari ya kupata jeraha mchezoni. Massage huondoa mkazo wa misuli (muscles tention) na hulainisha tishu laini za mwili hivyo huzuia hatari ya kupata jeraha mchezoni. Pia huzuia kuvimba sehemu zinazogongwa wakati mchezaji akiwa mchezoni.
5. Huondoa uchovu baada ya mchezo. Baada ya misuli kufanya kazi kwa kitambo fulani huchoka, kuchoka kwa misuli hupelekea pia kuchoka kwa mwili wote hivyo, Massage ya Wanamichezo huwasaidia wachezaji kupumzika mara mbili zaidi ya kupumzika kwa kawaida. Hii ni kwa sababu massage huzalisha endorphin hormone ambayo huleta furaha kwa mtu.
6. Husaidia kuondoa sumu katika misuli. Baada ya misuli kufanya kazi katika mchezo kiasi kikubwa cha lactic acid hujirundika katika seli za misuli. Hali hii hupunguza nguvu ya misuli na kusababisha mchezaji kukosa ufanisi katika mchezo.
@happinessmassage
✓ http://instagram.com/happinessmassage
✓ http://facebook.com/happinessmassage1
Happiness Massage, We Bring Back Your Happiness
0715343161 / 0756343161
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni