Massage ni ukandaji na usuguaji wa sehemu ya mwili (ngozi, tishu, misuli) kwa kutumia mikono au mashine maalumu. Huduma hii hutolewa kwa lengo la:-
Kuondoa maumivu katika sehemu fulani ya mwili.
>Kulainisha misuli iliyokaza.
>Kuondoa uvimbe.
>Kuondoa uchovu wa mwili.
Kutibu jeraha.
>Kurelax.
>Kutibu saratani kwa kuondoa seli mfu.
Kuondoa maumivu katika sehemu fulani ya mwili.
>Kulainisha misuli iliyokaza.
>Kuondoa uvimbe.
>Kuondoa uchovu wa mwili.
Kutibu jeraha.
>Kurelax.
>Kutibu saratani kwa kuondoa seli mfu.
>Kuchochea ufyonzwaji wa madini ya Kalsiam na Fosforas ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa.
>Massage ni huduma ambayo hutolewa kwa watu wa umri wowote na rika zote. Kuna aina mbalimbali za Massage, kila aina ya massage ina umuhimu wake wa kipekee katika mwili wa binadamu. Huduma ya Massage hutolewa na Wataalamu ambao hutumia maarifa yao kwa ustadi ili kutimiza lengo husika la massage.
Umuhimu wa Massage kwa Binadamu
1. Massage inaboresha mzunguko wa damu mwilini . Massage hudaidia kuondoa vikwazo (kama vile lehemu/cholesterals) katika mirija ya damu hivyo huifanya damu itiririke kwa urahisi. Pia
hot massage
inasababisha
Vasodilation- kutanuka kwa mirija ya damu, hali hii pia huifanya damu ipite kwa urahisi katika mirija na kuzifikia ogani na tishu zote mwilini.
2. Massage huboresha afya ya ngozi na Mfumo wa Utoaji takamwili . Massage huondoa tabaka la seli zilizokufa na kuipa ngozi mwonekano bora. Pia husaidia kufungua matundu ya vinyweleo yaliyoziba na kurahisisha utoaji wa jasho.
3. Massage huimarisha afya ya mifupa . Massage huchochea ufyonzwaji wa madini ya Kalsiam na Fosforas ambayo yana mchango mkubwa katika afya ya mifupa. Watoto wanaofanyiwa massage mara kwa mara si rahisi kipata matatizo ya mifupa kama vile
matege.
4. Massage inaondoa maumivu ya kichwa na msongo wa mawazo.
5. Massage hupunguza hatari ya kupata magonjwa hatarishi kama kiharusi, saratani na kisukari.
Bado wataalamu wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali juu ya massage ili kujua manufaa zaidi yatokanayo na huduma hii kongwe ambayo ni tiba asilia kwa matatizo mbalimbali.
DONDOO MUHIMU KUHUSU MASSAGE
1. Massage inaweza kufanywa na mtu yoyote iwapo atapata maelekezo kutoka kwa wataalamu.
1. Massage inaweza kufanywa na mtu yoyote iwapo atapata maelekezo kutoka kwa wataalamu.
2. Sio kila ugonjwa wa saratani unatibika kupitia massage, kuna aina mbalimbali za saratani.
3. Massage inarudisha hamu ya kula kwa watu waliopoteza hamu ya kula.
4. Massage inapunguza hatari ya kupata majeraha katika michezo. Mwanamichezo anayefanya massage mara kwa mara si rahisi, kuvimba ovyo hata kama amegongwa sehemu ya misuli. Hii ni kwa sababu misuli yake inakuwa laini na hivyo kukubali mijongeo kiurahisi.
5. Ni vizuri mama kumfanyia mtoto wake Massage, hasa baada ya mtoto kuamka au kabla ya kulala. Massage inaimarisha afya ya mtoto na kumfanya mwenye furaha muda wote.
6. Massage huwasaidia wazee kutembea kwa urahisi.
Maumivu ya mgongo hutibika kwa urahisi kupitia Massage hususani kama maumivu hayo yanatokana na mkandamizo wa misuli au neva. Kama maumivu ya mgongo yanasababishwa na pingili za uti wa mgongo Muone mtaalamu.
Maumivu ya mgongo hutibika kwa urahisi kupitia Massage hususani kama maumivu hayo yanatokana na mkandamizo wa misuli au neva. Kama maumivu ya mgongo yanasababishwa na pingili za uti wa mgongo Muone mtaalamu.
7. Massage pia humsaidia mama mjamzito kumuondolea uchovu, maumivu ya kiuno, na husaidia sana kupunguza maumivu ya Uchungu na kumfanya ajifungue kwa urahisi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni