- Massage ya kichwa huboresha mzunguko wa damu kichwani, na kuwezesha damu nyingi iliyo safi(yenye oksijeni) kunawirisha afya ya ubongo na ukuaji mzuri wa nywele.
- Huondoa sumu zilizorundikana katika sehemu za kichwa. Miili yetu huzalisha sumu mbalimbali ambazo hutolewa kupitia njia za utoaji takamwili (mkojo na jasho). Hata hivyo si kiasi chote cha sumu ambacho hutolewa kuna kiasi kidogo cha sumu hujikusanyaa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani. Hivyo Massage ya Kichwa husaidia kuondoa mlundikano huo wa sumu. Pia massage ya kichwa uchochea mtiririko wa mfumo wa limfu(lymphatic system) na hivyo husaidia uondoaji wa sumu(toxins) mwilini.
- Massage ya kichwa huondoa maumivu ya kichwa. Mara nyingi maumivu ya kichwa husababishwa na mkao mbaya au mvutano wa misuli. Massage ya kichwa huweka sawa mkao wa misuli na hivyo kumaliza kabisa tatizo la maumivu ya Kichwa.
- Huondoa usingizi na uchovu ambavyo ni dalili za msongo wa mawazo.
- Huboresha uwezo wa kutunza kumbukumbu.
Ijumaa, Oktoba 6
Faida za massage ya Kichwa/ head massage
Massage ya Kichwa ina umuhimu mkubwa katika kuboesha afya ya binadamu, hasa ukuzingatia kuwa ni sehemu iliyobeba kiungo muhimu katika mfumo wa fahamu. Massage ya kichwa ikifanywa kitaalamu kwa kutumia mafuta maalumu ina faida zifuatazo:-
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni