HISTORIA YA MASSAGE Historia ya massage(uchuaji) inatokea mbali takribani miaka 5000 iliyopita miaka ambayo massage(uchuaji) ilikuwa ni njia kuu katika matibabu ya magonjwa mbalimbali.Si magonjwa ya viungo tu bali pia hata magonjwa mengine Michoro ya mapangoni inayopatikana sehemu mbalilmbali Duniani ni ishara/dalili tosha inayothibitisha kuwa tiba hii kongwe(ya massage) ilianza miaka
mingi iliyopita.Kabla ya yote Ifahamike kwamba MISRI ni miongoni mwa mataifa ya mwanzo kabisa Duniani kutumia tiba hii ya massage(uchuaji) kuponya magonjwa mbalimbali.
Mataifa mengine ya mwanzo kabisa kutumia tiba hii ya massage(uchuaji) Duniaini ni China,Thailand,India,Japan,Korea,Rome na Ugiriki. Kuthibitisha hili,Mnamo miaka 2700 K.K(Kabla ya kuzaliwa kwa Kristo) kitabu cha kwanza kuhusu Massage kiliandikwa nchini CHINA.Kitabu hiki kilichofahamika kama “The Yellow Emperor’s Classic Book of Internal Medicine’’ kiliandikwa kwa lugha ya kiingereza kwa mara ya kwanza mwaka1949(Miaka 4649 baadae).Taratibu/Njia za matibabu kupitia massage za Kichina zinatokana na kanuni ya kwamba Magonjwa na Maradhi katika mwili wa binadamu husababishwa na upungufu/kutokuwa sawa kwa nishati(nguvu) katika njia maalumu mwilini ambazo zinawakilisha mfumo wa fiziolojia.
Miaka 2500 iliyopita Michoro iliyopo kwenye makaburi ya MISRI inaonyesha utamaduni wa massage(uchuaji) ulikuweopo nchini MISRI tangu enzi hizo.
Miaka 1500 na 500 India iliochapisha maandishi ya kwanza kuhusu massage(uchuaji),hata hivyo inakadiriwa kuwa Utamaduni wa tiba ya Massage(uchuaji) nchini INDIA ulianza tangu miaka 3000 K.K.
Katika nchi ya Japan tamaduni ya kutumia massage(uchuaji) kama njia ya kutibu magonjwa ilianza takribani miaka 1000 K.K.Japan ilijifunza njia hii ya massage(uchuaji) kutoka Kwa Wachina.Walitumia njia hii ya massage(uchuaji) kwa lengo la kuongeza nguvu katika mwili wa Mgonjwa.Walitumia tiba hii ya massage(uchuaji) kwa kutumia vidole,kiganja,kidole gumba bila kutumia sindano,na iliweza kurudisha nguvu kwa mgonjwa na hatimaye kupona kabisa.
Pia mnamo miaka ya 800 K.K na 700 K.K Wanafalsafa na Wanamichezo wa Ugiriki walianzisha tiba hii ya massage(uchuaji).Tiba hii ilianzia mashariki ya UGIRIKI na hata ikaenea hadi magharibi.Wanamichezo wa Ugiriki walitumia massage(uchuaji) kama njia bora ya kuweka miili yao sawa kabla ya kuanza Mashindno. Hadi ilipofikia karne ya tano K.K Wagiriki walianza kuitumia tiba hii ya Massage(uchuaji) kutibu majeraha na magonjwa mengine ya viungo.Tiba hii ya Massage iliambatana na kufanya mazoezi,kula mlo kamili,kupumzika na kupata hewa safi kwa ajili ya kuuweka mwili katika hali ya afya njema. Tiba ya massage(Uchuaji) inaingia Rome. Baada ya kuenea kwa Tiba ya massage(uchuaji) nchini UGIRIKI mwishowe ilienea hadi Rome katika miaka ya 200 na 100 K.K. Tunapozungumzia Tiba ya Massage(uchuaji) nchini Rome hatuwezi kumsahau Dk.Galen ambaye aliazisha tiba hiyo kwa watawala mbalimbali.Alitibu majeraha na matatizo ya viungo kupitia tiba hii ya Massage(uchuaji).Tiba hii ya massage ina manufaa makubwa kwa kutibu magonjwa mbalilmbali. (uchuaji) mara nyingi ilikuwa inatolewa katika maeneo ya wazi,ambapo Wataalamu na wanafunzi waliweza kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya viungo. Wanasayansi asilia walifanya kazi kubwa kuboresha tiba ya massage ili iweze kuleta manufaa zaidi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni