Alhamisi, Agosti 25

JINSI MASSAGE INAVYOTIBU MSONGO WA MAWAZO



Msongo wa mawazo(stress) ni hali inayotokea kwa mtu baada ya kukumbana na tatizo fulani lisilokuwa zuri katika maisha yake. Hali hii humfanya mtu ajisikie mpweke,aliyeuzika na kukosa
furaha kabisa na hata kukosa hamu ya kula.Mara nyingi msongo wa mawazo hutokea kwa Vijana,lakini muda mwingine na kwa wazee pia.Msongo wa mawazo usipopatiwa
Ufumbuzi,hupelekea SIMANZI,ambayo ndiyo hali mbaya zaidi. Watu wengi hupata msongo wa mawazo lakini hawafahamu hali hiyo ndio msongo wa mawazo.Zifuatazo ni Dalili zinazoweza kuashiria msongo wa mawazo. 1.Maumivu ya kichwa 2.Uchovu 3.kukosa hamu ya kula 4.Kujihisi mpweke 5.kushindwa kufanya kazi zako za kawaida.  SABABU ZINAZOPELEKEA MSONGO WA MAWAZO Kuna sababu mbalilmbali zinazopelekea Msongo wa mawazo......
Sababu hutofautiana kutoka mtu mmoja na mwingine.Zifuatazo ni sababu zinazopelekea Msongo wa mawazo.
 1.Kufeli Mitiahani Mtu anapopata matokeo mabaya ya mitihani yake kinyume na alivyotarajia anaweza kupata msongo wa mawazo.
 2.Kuondokewa na mzazi/wazazi au mlezi/walezi au mtu wa karibu kama vile mwenza,ndugu, rafiki n.k huweza kumfanya mtu apate msongo wa mawazo.
 3.Usaliti katika Mapenzi Hii ni sababu kubwa kwa vijana inayopelekea msongo wa mawazo.Mtu aliyeasalitiwa huwa katika hali ngumu ya kihisia nahivyo kumfanya apate Msongo wa mawazo.Unapokosekana Ushauri kwa mtu wa namna hii huweza kumfanya achukue maamuzi mazito hata ya kujiua,na hii imeshuhudiwa mara nyingi sana ikitokea.
 4.Matatizo ya kifamilia Panapotokea matatizo ya kifamilia kama vile ugomvi au malumbano na usipofikiwa muafaka huweza kutokea msongo wa mawazo pia. Sababu nyingine zinazopelekea Msongo wa mawazo ni: Mikwaruzano na watu,Hofu ya tukio linalotarajiwa kama vile Mtihani,Kesi Mahakamani n.k. 

ATHARI ZINAZOTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO 
1.KIFO Msongo wa mawazo huweza kupelekea kifo kama mhusika hatochukua hatua za kuiondoa hali hiyo au kama hatopatiwa suluhisho.Mfano mwaka 2013 kuna mwanafunzi aliyejiua kutokana na kupata matokeo asiyoyatarajia katika mtihani wake wa kidato cha nne.Hii bila shaka imetokea na msongo wa mawazo.

2.KUDORORA KWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KIUJUMLA. 
Kutokana na hali aliyokuwa nayo mtu mwenye msongo wa mawazo ni vigumu sana kufanya kazi na hata kama atafanya bado hakutokuwa na ufanisi.Hali hii hupelekea kushuka kwa shughuli za uzalishaji na hivyo huathiri hali ya uchumi.

3.MSONGO WA MAWAZO HUPELEKEA MAJONZI YA MUDA MREFU KWA MUHUSIKA. Kama msongo wa mawazo utaendelea kuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa suluhisho,inaweza kupelekea majonzi ya muda mrefu hali ambayo husababisha afya ya mhusika kuzorota. SULUHISHO LA MSONGO WA MAWAZO. Kabla sijaeleza kuhusu suluhisho la msongo wa mawazo,ningependa ufahamu kwanza.Kuna Njia tofauti zinazotumika kuondoa msongo wa mawazo.Njia hizi hutegmea ukubwa wa msongo wa mawazo. Kwa msongo wa mawazo wa kawida,njia zifuatazo zinaweza kumaliza kabisa tatizo hilo.

1.Massage ni Suluhisho bora kabisa katika  kuondoa Msongo wa mawazo. Kwa nini? Kwa sababu Wataalamu wa Massage(Uchuaji) wana ujuzi wa kutosha wa jinsi ya kushughulika na Mtu Mwenye Msongo wa mawazo kwa njia zote mbili(Kimwili na Kiakili). Na hii ndio tiba bora kwani mtu mwenye Msongo wa mawazo anaathirika kimwili(uchovu/kukosa nguvu) na kiakili.Wataalamu wanaotoa Huduma hizi za Massage(Uchuaji) kama vile Happiness Massage Services wanatumia Maarifa ya Fiziolojia na Saikolojia ili kuleta ufanisi katika tiba hii ya kuondoa Msongo wa Mawazo.Kitu cha kwanza kinachoathirika ni akili na baadae mwili hufuatia. Wataalamu wa Massage Hutumia mbinu muafaka ya kuanza kuondoa tatizo lililopo katika akili(ambalo huwa mawazo, huzuni, kujiisi mpweke, kufikiria mambo mabaya kama vile Kujiua) na baada ya kumweka mtu sawa kiakili Ndipo tiba ya Mwili inafuata.

Njia nyingine za kutatua tatizo hili la msongo wa mawazo n

2.Kutafuta mtu wa kuongea nae badala ya kukaa peke yako.

3.Kufanya mazoezi ya viungo.
Husaidia kuweka akili sawa na hivyo kurudi katika hali ya kawaida.

4.Kula mlo kamili. Mara nyingi mtu mwenye msongo wa mawazo hukosa hamu ya kula, na hali hii ya kukaa bila kula ndio huongeza zaidi tatizo, hivyo inashauriwa kujilazimisha kula. Ikiwa haya yote hayo yamefanyika na hakuna matokeo chanya, Msaada wa kitaalamu unahitajika kwa haraka kabla ya kuleta madhara zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni