Mtoto ni tunda bora linalotokana na Mti wa Ndoa. WanaNdoa walio wengi Duniani hujikuta katika furaha isiyo na kifani wanapopata Mtoto/Watoto. Wapo wanaosema kuwa Mtoto ni burudisho la Macho ya Wanandoa na hili si Uongo ni kweli kabisa.
Mtoto anahitaji apatiwe Huduma nyeti sana ambayo kutokana na huduma hiyo nyeti na muhimu ndiyo itakayomjengea msingi mzuri katika maisha yake yote atakayoishi hapa duniani. Huduma hiyo si nyingine bali ni malezi. Na si malezi tu bali Ni malezi bora. Malezi yana maana kubwa sana kuanzia Kumpatia mtoto chakula bora, Mavazi, Huduma bora za afya na kuhakikisha kuwa Mtoto anakuwa na furaha, ni miongoni mwa vipengele vya Malezi.
JE,WAJUA?
Massage humuongezea Mtoto Furaha na si Hivyo tu, Bali pia Huboresha Afya ya Mtoto. Kama ulikuwa haufahamu basi kuanzia leo fahamu hivyo. Makala hii itajikita zaidi katika Kuzungumzia Umuhimu wa Massage Kwa Mtoto mdogo. Massage ina umuhimu mkubwa katika kuboresha Afya ya Mtoto na Kumuongezea Furaha.
“Unapomfanyia Mtoto wako Massage,Bila shaka unausisimua Mfumo wa Fahamu”<Maneno haya Yalitamkwa na Dr.Tiffany Field kutoka Taasisi ya Uchunguzi ya Chuo Kikuu cha Miami (Marekani), Katika kitengo cha Shule ya Matibabu.
Bila kwenda mbali zaidi Massage humletea mtoto Mambo yafuatayo.
1.Humfanya mtoto apate Usingizi Mzuri. Hii ni kutokana na Masaage hulainisha viungo vyake na kumfanya mtoto awe katika hali nzuri ya kimwili.
2.Inaboresha Afya ya Mtoto. Kama ilivyotanguliwa kuandikwa kwamba Massage kwa mtoto husisimua mfumo wa fahamu. Msisimuko huo wa mfumo wa fahamu husababishwa kuzalishwa kwa Serotonin, ambayo ndiyo huleta furaha.Serotonin ndiyo pia inayosaidia kuongeza raha katika Tendo la Ndoa. Hii husaidia kupunguza mapigo ya moyo kwa mtoto na kumwacha mtoto akiwa na furaha muda wote.
Karibu Happiness Massage Tuboreshe Afya ya mtoto wako na kurejesha furaha yenu.
0715343161
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni