Jumatano, Agosti 17

Tiba ya chunusi, Fahamu kwa undani hapa.

  Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wa mataifa yote na wa umri wote. Ugonjwa uliozoeleka zaidi ni ule unaowapata vijana wakiwa kwenye umri wa balehe. Zaidi ya asilimia 70 ya vijana wa umri huu hupata chunusi. Chunusi huwapata vile vile watu wenye umri mkubwa na, vichanga wengine hupata chunusi kutokana na mama zao kuwarithisha homoni kabla tu ya kuzaliwa. Ukurasa huu utajadili chanzo cha chunusi katika mwili wa binadamu, aina za chunusi na hatua zinazoweza kuchuliwa ili kuepukana na chunusi.


    Katika mwili wa binadamu, chunusi huonekana zaidi maeneo ya usoni, mgongoni, kifuani, mabegani na shingoni. Kutegemeana na uwingi wa chunusi hizo, mwathirika huweza kunyanyasika kimawazo na kupata makovu juu ya ngozi yake. Kuna dawa za kutibu chunusi ingawa ni ugonjwa unaoweza kujirudiarudia. Chunusi huondoka polepole sana na wakati mwingine chunusi mpya huanza kujitokeza kabla nyingine kupona kabisa. Ni ugonjwa unaotakiwa kupewa tiba ya mapema ili kuepuka kupata madhara ya kudumu.

Chanzo Cha Chunusi Ni Nini?
 Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles). Picha hapa chini inaonyesha muundo wa kitengo kimoja cha kinyweleo (pilosebaceous unit). Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.
    Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.
    maycohezDawa ya chunusi bei gan @happinessmassage
    happinessmassageInategemea Na kiwango cha kuasilika kwa ngozi yako ya uso tupigie 0715 34 31 61 au whatsapp Kama upo mkoani tukutumie dawa karibu sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni